Monday, May 28, 2012

MKONGA WA MAWASILIANO WAENDELEA KUTANDAZWA MJINI HAPA

0 comment
Mtambo wa kuchimba na kutoboa njia za kutandaza kebo za Mkonga wa mawasiliano ya Internet
.
Shughuli ya kutandaza mkonga huo ikiendelea na mradi huu ukikamilika hadithi za mambo hayaendi zitasahaulika asa kiutendaji.
Wataalam  wa kuunganisha kebo za mawasiliano wakiendelea kutandaza mkonga wa TTCL chini ya ardhi kuelekea ofisi za wizara ya kazi na maendeleo ya Vijana zilizopo Mtaa wa Miembeni Mjini hapa.

Sunday, May 27, 2012

TUNATOA POLE KWA MSIBA WA MAREHEMU SULEIMAN BWIKIZO WA KASHAI ULIOTOKEA HII LEO MJINI BUKOBA NA MAZISHI YATAFANYIKA JUMATATU TAREHE 28-5-2012 KIJIJINI KWAKE IZIMBYA

3 comment
Marehemu Suleiman Bwikizo (kulia)
Marehem Bwikizo aliwahi kuwa ofisa masoko wa bukoba Mjini mpaka anastaafu.
Mazishi yatafanyika Jumatatu saa 8 mchana kijijini kwake Izimbya Bukoba vijijini.

HALI YA VURUGU ZANZIBAR IKIWA IMEANZA KUA SHWARI WADAU MBALI MBALI WATOA MAONI YAO KUFATIA KITENDO VYA KUCHOMA MOTO KANISAA

0 comment
Hali ikiwa shwari hii leo.
Maelfu wa Wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar JUMIKI, wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa Serikali ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru, ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongozwa na Kiongozi wa Jumuiya hiyo, Sheikh FARID HADI AHMED na viongozi wengine.




MAONI YA WADAU MBALIMBALI
  • Christopher Kaijage kuna nini katika muungano huu .??kama ni suala la usalama sisi tunayo majeshi ya kulinda usalama sio mpaka zanzibar iwe ndani yetu hata hivyo bado tunawaonea zanzibar tuwaache wajitawale kwani kwa sasa wanawasomi wa kutosha wanazo maligafi za kujitunza na pia sijui kama itakuwa safi kama wakitumuliwa hapa kariakoo maake ndo inawabeba , nawashauri ndugu zangu viongozi wapeni uwezo zanzibar wajitawale kabla suala la udini alijaanza "jihad"inanukia sasa

  • Prudens Rweyongeza Sasa Makanisa yanahusika vipi na kero za Muungano??? Watu wanatumia fursa hizi za machafuko kutekeleza mambo yao ya chuki dhidi ya wenzao! Hizi dhambi zitawatafuna hata kama ikitokea wakajitenga, kamwe hawataishi kwa amani!
     
      
     Statement  ya Zitto Kabwe

1 .Vurugu za Zanzibar ni 'unwanted distractions' katika mchakato wa kuandika katiba mpya.

2. Hakuna namna vitendo hivyo vinaweza kuhalalishwa na kutetewa lakini ni matokeo ya muda mrefu ya 'superficial attempts at dealing against groups with ulterior motives.

3. Rais Ali MohamedShein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti vurugu hizo,na kuanza mzungumzo na pande zote.Hiki sio kitendo cha kudharau kabisa

4. Muungano wetu ni sacred na tumetoka mbali kushindwa sasa kuulinda, 'not when we are so close at having an everlasting formula'

5. Waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara moja. Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa.

6. Zanzibar Political leaders and public opinion makers must engage the Zanzibaris into a serious and objective dialogue about the future of Zanzibar within or outside the Union.

PICHA YETU YA LEO.

2 comment
Mdau Sawia Sadru akiendelea na shughuli zake.

CAMERA YETU PANDE ZA KIROYERA BEACH JUMAPILI YA LEO

2 comment
Bi Zakia akiwa ametulia na ufukweni na mwanae.
 Anaonekana akiendeleza mbili tatu Bi Zakia na shost wake
Pande za kiroyera beach jumapili ya leo wadau wakiendeleza maisha.
Kwa pamoja wadau wakimalizia jumapili yao ufukweni.
Maisha ni kuchagua ,hapa ni Mtumbwini wadau wakila bata ....!!

Saturday, May 26, 2012

GARI TOYOTA HIACE INAUZWA IPO KATIKA HALI NZURI NA INAFAA

0 comment
Gari hili linauzwa lipo katika hali nzuri linafaa kwa  kwa kukabiliana na hali yoyote ya barabara.
Gari nisafi mie mwenyewe wadau nimeipenda ila uwezo wa kuinunua ndio sina
BEI YAKE NI TSH 8,000,OOO/=SHILINGI MILIONI NANE TU ZA KITANZANIA!!!!

MAWASILIANO PIGA SIMU +255 755 017061 AU +255 754 505043 NA +255 713 397242

HOJA YA KILIMO KWANZA NA WAKULIMA WA KIGENI

0 comment

Na E.Sabuni.
Mimi ni mtanzania ninayejivunia utanzania wangu. Naomba kuongelea hili swala la kilimo kwanza. Mimi kama mimi naomna hili swala linapelekwa kisiasa kuliko ilivyotegemewa. Jamani tunaposema kilimo kwanza mara Tenda za matrekta zimeishatoka haraka sana na watu kuanza kuvuna hela isiyokuwa na jasho kwa kutuingizia vitu vibovu kwa kweli inasikitisha sana. Utasemaje kilimo kwanza wakati wakulima wenyewe ujawapa mbinu za hicho kilimo kwanza mnachosema, mtanatangaza kilimo kwanza ndo mfumuko wa bei za vyakula kwanza kweli inasikitisha. Pili kwa nini serikali haikai ikafikiria hivi vitu wanavyofanya vinaenda kunyume na matakwa ya wanainchi? Sawa kilimo kwanza mmeturetea power tiller, power tiller zenyewe vimeo hasa hizi kubwa kwanza mbovu, pili ulaji wa mafuta kupita kiasi kila mtu anazikimbia anaona bora kutumia jembe la mkono kuliko hizo power tiller sijui trekta.

Napenda kuuliza kwanini tuna wataalamu wa kilimo? Wote wamejazana hapa Dar, Arusha, Mwanza  napo ni ofisi za mjini sio vijijini hawataki kwenda mikoa mingine kisa haina maendeleo na miundo mbinu mibovu eti kilimo kwanza kilimo kwanza mjini uliona wapi? Ifike wakati serikali ipeleke wataalamu mikoani hasa ile inayozalisha vyakula kwa wingi sio kuweka watu wa chin indo wanafaa kufanyakazi vijijini wakati wa mijini wanakula posho ambazo hawajazifanyia kazi na kupeana safari za nje ovyo ovyo basi hizo safari wapewe watu wanaofanyakazi mikoani wakajifunze kuliko wanaokaa mini.

Nasikitika kuona Tanzania kuona eti tunamfuko wa bei za vyakula kweli. Mimi binafisi naomba kilimo kwanza neno lifutwe liwe tumbo kwanza. Nimesikia eti serikari ya Marekani wametoa hela kwa ajili ya kilimo kwanza hizo hatutaziona make ndo kwanza zaidi ya kuona matrekta ya mchina yanayowaumiza wananchi yanakula mafuta kama hayana akili nzuri na ubovu kila mara  badala ya kumsaidia mwananchi yana muumiza.


HOJA NYINGINE (WAKULIMA WA KIGENI)
Nikirudi tena kwenye hoja ya wakulima wa kigeni hivi kweli niwakati wake? Mimi naona sio wakati wake naona mnatuletea watu wakuacha wametualibia ardhi yetu na wengine kuzamia moja kwa moja make nchi yetu ni shamba la bibi watu wanachuma na kuondoka. Pili kuwakumbatia wakulima wakigeni na kuwapa ardhi kulima mazao ambayo wakulima wakawaida wakipewa mafunzo watalima kwa utaalamu zaidi. Mfano nasikia kuna wachina wanalima mboga za majani aina zote pale mto Ruvu na ujue wao wanauelewa  wa juu kwa maswala ya kilimo hivi kweli ni haki? Hivi kweli wakulima wadogo wadogo wataweza kupata soko? Make nasikia wanaiginza fuso tatu kila siku pale kariakoo na wameteka mahoteli ya hapa Dar yote  hivi unafikiri sisi umasikini utakakwisha make kila mtu akipata sehemu anataka aibe kwanza. Na hiyo itakuwa dili ya mtu kawaweka hapo anapata 10% yake. Lakini itafika wakati wananchi tutaamua tutawafukuza kwenye ardhi yetu.

KUTOKA KATIKA PAGE YA ZITTO KABWE NIMEICHUKUA KAMA ILIVYO

0 comment
 Kesho Jumapili tarehe 27 Mei mwaka 2012 nitakutana na Watanzania wanachama na wapenzi wa CHADEMA wanaoishi Marekani. Mkutano utafanyika katika Jimbo la Maryland kama ilivyokwisha tangazwa hapo awali.

Katika mkutano huu wa kwanza na wa aina yake tutazindua uandikishaji wa wanachama wa CHADEMA kwa Watanzania wanaoishi Marekani. Pia tutazungumza masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu. Masuala ya kwanini nchi yetu haiondokani na umasikini licha ya utajiri wa rasilimali uliopo nchini, masuala ya namna gani tunajiandaa na uchumi wa gesi asilia na nafasi ya Watanzania waishio nje katika maendeleo ya Taifa.

Tutazungumza kuhusu uandikaji wa Katiba mpya na namna haki za Watanzania wanaoishi nje zitakavyoingia kwenye Katiba ikiwemo haki ya kupiga kura na hata haki ya kuwa na Uraia wa pili.

Ninapenda kuwakaribisha katika mkutano huu muhimu sana. Njooni tuzungumze. Njooni tujadiliane. Wasiliana na viongozi wa chadema Marekani kwa maelekezo zaidi.

Thursday, May 24, 2012

Senene wamiminika ile mbayaaaaaa!!!!!Bei ni fololo gharama kubwa ni kuwaandaa!!!!!!

3 comment
Mdau muuza senene akiendelea kuchuhuza senene wake....



Kadanke akiwa mawindoni
Mawindoni kadanke akinyatia taratibu....!!
Wakiwa tayari wamemenywa
Barabara  ya Jamuhuri haipitiki kutokana na wingi wa watu.
Ni hali ya wadaub na biashara ya Senene.

Wednesday, May 23, 2012

AJALI YA PIKIPIKI NA COROLLA JIONI YA LEO MAENEO YA UNITED KINGDOM WAREHOUSE

0 comment

Gari aina ya Corolla lenye nambari T 851 BLF  lililokua likijaribu kupita kwa ku  overtake kwakutokea chini  kabla ya kukutana na mwendesha pikipiki na kumvaa mzima mzima.
Pikipipi iliyogongwa ikiwa mikononi mwa polisi katika eneo la tukio huku simu zikipigwa kuitaji msaada zaidi.
Mashuhuda wa ajali hii wakiendelea kunogesha maongezi
Ajali hii imetokea jioni ya leo barabara ya Kashozi njia panda ya kishenge( Machinjioni) mjini hapa.

MBONI SHOW KUANZA KURUKA NDANI YA EATV MEI 31, 2012

0 comment
 Mtangazaji wa Kipindi Kipya Mboni Show, Bi. Mboni Masimba kinachotarajiwa kuruka hivi karibuni katika sresheni ya EATV akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa kipindi chake. Pembeni yake ni msimamizi wa kipindi hicho Bw. George Tyson na msimamizi wa vipindi vya EATV. Kipindi hichi cha Mboni Show  dhima yake ni kuburudisha, kuelimisha, kufundisha, uonya, uadhibu na kuelekeza jamii ya Watanzania inayokabiliwa na changamoto nyingi katika maisha ya kila siku. Na pia kipindi kinakusudia kuleta mapinduzi makubwa katika muendelezo wa vipindi vya mahojiano.
Meneja wa Vipindi kutoka EATV akizungumza katika uzinduzi huo wa kipindi cha Mboni Show kinachotarajiwa kuanza kuruka Mei 31 ndani ya EATV.
Msimamizi wa kipindi cha Mboni Show Bw. George Tyson akielezea ubora wa kipindi hicho.
Waaandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo
 Waandishi wakiwa kazini.
 Mtangazaji wa Kipindi Kipya Mboni Show, Bi. Mboni Masimba akiteta jambo na msimamizi wa Vipindi wa EATV. 
Lakini pia anapenda muziki, mitindo na ni mjariamali anayemiliki kampuni yake binafsi iitwayo 'CHOCLATE PRINCES' ambayo inaendesha duka la mavazi, vipondozi na viatu vya kike lakini pia ndiyo waandaaji wa kipindi kipya cha luninga 'THE MBONI SHOW'. Picha zote na www.kajunason.blogspot.com

WAKULIMA WA KILIMO CHA KISASA KUTOKA NCHINI AFRIKA KUSINI WATEMBELEA TANZANIA

0 comment
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Africa Century 4 Development (CC) Fred Simon akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kuwakaribisha wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka makampuni 13 ya nchini Afrika Kusini ambao wamekuja Tanzania kwa ajili ya matembezi ya kujifunza mbinu mbali mbali za kilimo na kuangalia fulsa za kuikwamu Tanzania katika mpango wa kilimo kwanza.
 Mkutano wa waandishi wa habari pamoja wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka Afrika Kusini.
Katibu Mtendaji wa Tanzania Youth Agriculture Foundation (TYAF) Bw. Gasper Mahekula akitoa maelezo machache ya taasisi yao mbele ya wakulima kutoka nchini Afrika Kusini pamoja na waandishi wa habari ambapo aliwakaribisha wageni hao kuwekeza katika kilimo.
Wa kwanza kulia ni Mtaalam wa Mambo ya Utawala wa Kilimo wa Kampuni ya IIQ ya Afrika Kusini Bw. Ockie Olivier ambaye ameongozana na wenzake wakifuatilia mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. Braam Coetnee (kushoto) wakiwa na mmoja ya wenyeji wao (katikati) pamoja na Kiongozi anayehusika na mambo ya nje ya Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. John Luscombe jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Africa Century 4 Development (CC) Fred Simon akifanya mazungumzo na waandishi wa habari mara baada ya mkutano jijini Dar es Salaam.
Kiongozi anayehusika na mambo ya nje ya Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. John Luscombe akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya mkutano jijini Dar es Salaam. Picha/www.kajunason.blogspot.com